About TCAA CCC

KUHUSU BARAZA

Baraza la watumiaji wa huduma ya usafiri wa anga Tanzania limeundwa kwa mujibu wa sheria ya usafiri wa anga sura ya 80 kama ilivyorekebishwa mwaka 2006, Madhumuni yake nikulinda na kutetea maslahi ya watumiaji wa huduma ya usafiri wa anga nchini. Baraza limeundwa ili liwe chombo kitakachokuwa kinawawakilisha watumiaji katika soko la usafiri wa anga.

 

MUUNDO WA BARAZA

Baraza linaundwa na wajumbe wasiopungua watano nawasiozidi kumi.  Waziri mwenye dhamana ya usafiri wa anga anamteua mwenyekiti wa baraza na wajumbe wanamchagua makamu mwenyekiti kutoka miongoni mwao. Wajumbe wa baraza ndio wanaosimamia utekelezaji wa majukumu na malengo ya baraza pamoja na mipango yote ya mikakati.

 

SECRETARIAT

Utekelezaji wa malengo na majukumu ya baraza unatekelezwa na kuendeshwa na secretariat yake. Katibu mtendaji wa baraza ndio mkuu wa secretariat akiwa na kazi ya kuhakikisha kuwa baraza linafikia malengo yake.  Katibu mtendaji anafanyakazi akisaidiwa na maafisa wengine waliopo kwenye secretariat. Ofisi za Secretariati ya baraza zinapatikana jingo la PPF gorofa ya saba, katika makutano ya barabara ya Samora na Morogoro.

 

 

Kazi Kuu za Baraza ni Kama Zifuatazo

 

1.    Kuwakilisha maslahi ya watumiaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa kushauriana na mamlaka husika (TCAA) waziri mwenye dhamana ya mambo ya usafiri wa anga katika mambo yanayogusa maslahi ya mtumiaji.

 

2.    Kupokea na kuwasilisha taarifa na maoni kuhusu maswala ya msingi ya watumiaji wa huduma za usafiri wa anga.

 

3.    Kuanzisha kamati za watumiaji katika kanda na  mikoa na kushauriana na kamati hizi.

 

4.    Kufanya mashauriano ya kina na wahusika katika sekta ya usafiri wa anga, serikali pamoja na makundi mengine ya watumiaji wa huduma ya usafiri wa  anga kuhusu maswala ya msingi na kero mbalimbali za watumiaji katika sekta.