Wajibu wa Mtumiaji

  • Mtumiaji ana wajibu wa kufuata maelekezo na kuchukua tahadhari ili kuweza kuzingatia usalama wa maisha yake awapo safarini.


  • Mtumiaji ana wajibu wa kuchagua chombo cha usafiri .


  • Mtumiaji ana wajibu wa kulalamika pale anapoona maslahi yake hayazingatiwi au pale anapopata madhara kwa kutumia huduma


  • Mtumiaji ana wajibu wa kuhakikisha bidhaa na huduma muhimu katika maisha ya kila siku zinapatikana


  • Mtumiaji ana wajibu wa kutafuta na kutumia taarifa kabla ya kufanya manunuzi ya huduma au bidhaa husika ili kuhakikisha wakati wote anafanya maamuzi baada ya kupata taarifa kamili kuhusu bidhaa au huduma husika


  • Mtumiaji ana wajibu wa kutumia huduma kwa jinsi zinavyotunza mazingira. Kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kuwa makini katika kuchagua na kutumia huduma na bidhaa.


  • Mtumiaji ana wajibu wa kufanya juhudi za kuwezesha maoni yake kufahamika kupitia vyama vinavyotetea maslahi ya Mtumiaji.


  • Mtumiaji ana wajibu wa kuimarisha nguvu ya ushawishi kwa kujiunga katika vyama vya utetezi wa mtumiaji ili kuwa na sauti katika kusimamia haki na maslahi ya mtumiaji