Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko ya Watumiaji

Mtumiaji wa huduma ya usafiri wa anga atalalamika kwa maandishi moja kwa moja kwa mtoa huduma anaehusika akiambatanisha vielelezo muhimu vinavyohusu lalamiko lake na kutuma nakala kwa Baraza. Endapo mlalamikaji hatoridhishwa na majibu kutoka kwa mtoa huduma, mlalamikaji anatakiwa kupeleka malalamiko Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) na kutuma nakala kwa Baraza. Kutuma nakala kwa baraza la ushauri wa huduma za usafiri wa anga kunalisaidia Baraza katika kufuatilia malalamiko ya mtumiaji katika ngazi husika na kuweka msukumo wa kupata majibu kwa mujibu wa sheria zilizopo. Baraza pia huandaa maoni ya kisheria kupitia Kamati ya Mambo ya watumiaji na Malalamiko.

Kwa Mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa Anuani:

Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma ya usafiri wa anga (TCAA Consumer Consultative Council)

Gorofa ya 7, Jengo la PPF House, Makutano ya barabara ya Samora na Morogoro.

Simu:  +255 22 2128290

Fax:     +255 22 2128291

Simu ya kiganjani: 0719 100 600

S.L.P     12242, Dar-es-Salaam, Tanzania.

Tovuti: www: tcaa-ccc.go.tz

Haki zenu. Maslahi Yenu. Ndio Lengo letu.

 

 

Complaint Form

DOCUMENT/Complaint_form.pdf